HABARI NA MIUJIZA
Idadi ya watu inayokadiriwa kufikia 10,000 walihudhuria na baadhi yao kufunguliwa katika uwanja wa Samora uliopo katika Manispaa ya iringa mjini.
Mkutano huo ulioongozwa na Askofu Boaz Sollo kutoka katika huduma ya OPC uliwakutanisha wakazi wa manispaa ya iringa na vitongoji vya jirani waliofurika ili kupokea miujiza yao.
Huduma hiyo iliyokuwa na lengo la urejesho na uponyaji kwa watu wote ambapo ibada zake hufanyika kila siku za Alhamisi na Jumapili katika ukumbi wa IDYDY ambao kwa sasa ukumbi huo umeonekana kuwa mdogo kutokana na idaidi ya watu kuongezeka.
Mmoja wa watu walioshuhudia kupata uponyaji kutokana na huduma itolewayo ya na OPC aliyetambulika kwa jina la Magdalena Ndege alisema kuwa baada ya kuhangaika kwa mda mrefu katika hospital nyingi ikiwemo kwa waganga zaidi ya 13 bila mafanikio kutokana na kusumbuliwa na kansa. Alipopata muujiza wake huo wa uponyaji baada ya kuombewa na Askofu Boaz Sollo kupitia huduma ya overcomers power center.
Bi Magdalena alisema anamshukuru Mungu sana kwa kuwa baada ya kufika katika Huduma ya OPC na kuombewa na Askofu Boaz Sollo ndipo aliporejea katika hali yake ya kawaida kwani aliharibika sana kutokana na kansa iliyokuwa inamsumbua.
No comments:
Post a Comment